Friday, October 8, 2010

BANGI, NIBANGUE MPAKA CHEEEEEEEEEEE!!!!

Bangi ni nini?

Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa ya kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.

Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, dawa, ganja, hashish, kijiti, marijuana, kaya blunt na mengineyo, ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka.

Watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.

Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu na huathiri afya.

Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani ya chai na wengine huchanganya kwenye chakula.

Athari ya bangi ni ipi?

Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.

Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, mawazo, anaridhika hata kama ana matatizo.

Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.

Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza mapigo ya moyo kutoka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.

Bangi huaribu mapafu, kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaku.

Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.

Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.





Tafiti za wanasayansi

Kumekuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.

Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.

Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.

Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.

Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.

Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.

Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.

65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.

Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika kwa figo na ini.

Watafiti wamebaini vijana wengine kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).

Baada ya kubaini hayo watafiti wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.
Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.

UTANIPA MAJIBU JUU YA HILI KAMA UTAFEEL.

KWA MAONI, MAWAZO JUU YA BLOG HII NA CHOCHOTE UTAKACHOSOMA PLEASE MDAU NITONYE KUPITIA BARUA PEPE ( E-MAIL) HIYO HAPO JUU.

Friday, October 1, 2010

MAMBO VIPI WAUNGWANA MPO POA???

LONG TIME MBAYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Me mzima wa afya na naendelea poa na kuchaplika hapa town. Ubize ulikuwa kiasi lakini si sana kiivyo kwani yapo mazuria ambayo nimekuandalia ya kuyafahamu na kujiuliza ili tuweza kusongesha gurudumu la maisha.

Ndani ya mjengo wa MOSHI FM kama kawa kama dawa mambo nayasongeshwa kwa sana tu, na kama upo kanda ya kaskazini ( Tanga,Manyara,Kilimanjaro na Arusha) unatusoma kwa 90.2. Pindi nazishona zile zile Mid-Morning Cruise jumatatu hadi ijumaa saa 2.00-5:00 asubuhi, The base kila jumatatu - alhamisi saa 7:00-10:00 mchana, Project 120 kila ijumaa saa 7:00-10:00 mchana, Nipe Nikupe kila jumamosi na jumapili saa 1:oo-4:00 asubuhi na Supreme countdown jumamosi saa 12:00-02:00 usiku.


Kama kawaida pia nakandamiza kama ticha wa masomo ya uandishi na utangazaji katika chuo kikongwe na maarufu cha udzungwa. Karibu ujiunge.

Mwana nimerudi kwa kishindo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sunday, July 18, 2010

CHEKI SWAGGAZ ZA PROJECT 120!!!!!!!!!!!!

HOT PINDI NDANI YA MOSHI FM 90.2

Hii ni shoo kali ndani ya redio moshi fm kila ijumaa saa 7 hadi saa 10 jioni, wengi hawakosi kuisikiliza sikjui wewe. The big host wa hot pindi hili ni Mzeiiyaaaa wa milazo. Mzazi usijaribu kusikiliza hutaacha.


Nyie watoto kwa makamuzi si mchezo mnafanya balalaaaa. Huyu ni Ntoly Mayombole baada ya mzuka aliamua kuvamia shoo kwa upande wa pili wa studio.




Hisia za mziki zinapogusa mahala penyewe hakuna mkubwa wala mtoto, bosi wala mfanyakazi na milazo tata ni raha raha raha mpaka mwisho mwisho!!!!!!!!!!. Mwenye shati la drafti nyekundu na nyeupe ni Meneja wa redio moshi fm, Bw Deus Mworia.




Mwenye Tshirt ya mistari ya bluu na nyeupe(kushoto) ni Dj Poggo na mwenye tshirt nyekundu (kulia) ni Dj Q. Machizi ambao wanawakilisha vema katika shoo hii kali pia wagonga pini ndani ya club laliga


Mwenyewe headphone ni host wa hot pindi la project 120 Mzeiyaaa wa milazo na kwa mabli ni madj's wakigonga pini kwa ushirikiano.


The host wa hot pindi "project 120" Mzeiiiyaaaaaaaa akichongana na Dj Poggo.

Usiache kusikiliza Moshi Fm kwa vipindi vikali baada ya marekebisho ya nguvu.








HAPPY BIRTHDAY MADIBA!!!!!!!!!

HONGERA MANDELA MUNGU AKUZIDISHIE UMRI

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 92, huku ulimwengu ukisherehekea kwa mara ya kwanza, "Siku ya Nelson Mandela Duniani" kwa heshima ya kiongozi huyo.


Viongozi wa kimataifa na watu wa kawaida nchini Afrika Kusini na nje ya nchi hiyo, wameahidi kujitolea kuhudumia jamii kwa dakika 67 katika ishara za kuadhimisha miaka 67 ya kiongozi huyo kushughulikia kisiasa.
Tangu kuondoka madarakani, Mandela amejitokeza hadharani mara chache tu. Juma lililopita alikwenda kwenye uwanja wa michezo wa Soccer City mjini Johannesburg, kuwapungia mkono mashabiki wa kandanda kabla ya kufunguliwa mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia, lakini hakubakia kutazama mchezo kwa sababu ya hali yake dhaifu ya afya.

Tuesday, June 22, 2010

AFRIKA BYE BYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wenyeji wa kombe la dunia, Afrika Kusini wametupwa nje ya fainali za kombe la dunia pamoja na kwamba walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa katika mechi yao ya mwisho.
Hata hivyo Vigogo wa ulaya Ufaransa wameliaga kombe la dunia wakishika mkia kwenye kundi baada ya Afrika Kusini kuwabebesha virago.
Wawakilishi wengine wa Afrika, Nigeria watabidi wajilaumu wenyewe kwa kuliaga mapema kombe la dunia, kutokana na nafasi nyingi za wazi walizozipoteza.
Nigeria ilihitaji ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Korea Kusini, lakini iliambulia sare ya magoli 2-2, yalifungwa na Kalu Uche kwenye dakika ya 12 na Yakubu kwa njia ya penalti kwenye dakika ya 69.
Matumaini ya Afrika yamebaki kwa timu za Algeria, Ghana na Ivory Coast.